22.8 C
New York

Mbappe acharuka akimkingia kifua Dembele

Published:

MEXICO CITY, Mexico

NAHODHA wa timu ya soka ya Taifa ya Ufaransa, Kylian Mbappe, amesema si sahihi kwa Ousmane Dembele kukosolewa kwa kiwango alichokionesha katika mchezo uliopita dhidi ya Senegal.

Ni katika mchezo ambao Ufaransa iliibuka na ushindi wa mabao 3-1, ambapo wengi hawakuridhishwa na uwezo wa staa huyo wa PSG.

Kuelekea mchezo dhidi ya Iraq, Mbappe amesema watu hawapaswi kusahau kuwa Dembele ni mshindi wa Ballon d’Or.

“Ousmane? Nimerudia mara mbili kuitazama mechi ile (ya kwanza). Kipindi cha kwanza, alikuwa bora zaidi kati ya washambuliaji wanne.

“Kipindi cha pili, mimi na Michael (Olise) tulikuwa bora zaidi, lakini bado alikuwa na mchango,” amesema Mbappe.

Related articles

Recent articles