LONDON, Uingereza
ARSENAL imefanikiwa kuinasa saini ya kipa wa Phoenix Blayney, ambaye pia alikuwa kwenye rada za Liverpool.
Kipa huyo mwenye umri wa miaka 16, amekuwa kwenye kiwango bora akicheza Larne ya Ligi Kuu nchini Jamhuri ya Ireland.
Baba yake, Alan, ndiye aliyethibitisha Arsenal kumsajili Blayney, akisema nyota huyo amesajiliwa baada ya kufaulu majaribio yake.
Hata hivyo, hatosaini mkataba wa soka la kulipwa hadi atakapotimiza umri wa miaka 17 ifikapo Novemba, 2027.
Mbali ya Liverpool, klabu nyingine ya Ligi Kuu ya England iliyokuwa ikimtolea macho ni Nottingham Forest.


