17.4 C
New York

Alonso aanza kuisuka Chelsea tishio

Published:

LONDON, Uingereza

CHELSEA walimaliza msimu wa 2025-26 wakiwa na machungu ya kukosa tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya (2026-27).

Sasa, baada ya kumaliza msimu huo wakiwa nafasi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi, kocha wao mpya, Xabi Alonso, ameanza kusuka mipango ya kurejesha heshima iliyopotea Stamford Bridge.

Chelsea chini ya Alonso imeshakamilisha usajili wa Geovany Quenda (Sporting Lisbon), Emanuel Emegha (Strasbourg) na Dastan Satpaev (Kairat Almaty).

Wakati huo huo, bado Blues wako kwenye mazungumzo na straika wa Juventus raia wa Serbia, Dusan Vlahovic.

Je, Alonso aliyetua Chelsea baada ya kufukuzwa Real Madrid atafanikiwa kurejesha heshima iliyopotea pale Darajani?

Related articles

Recent articles