LOS ANGELES, Marekani
VURUGU zilizotokana na shangwe la ubingwa wa New Knicks ya Ligi Kuu ya Kikapu ya Marekani (NBA) zimesabaisha kifo cha shabiki, huku mabasi kadhaa yakichomwa moto.
Kwa mujibu wa ripoti, aliyeuawa kwa kupigwa risasi ni kijana mwenye umri wa miaka 17 katika mitaa ya Times Square.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa vurugu zilizotokea mitaani muda mfupi baada ya Knicks kuifunga San Antonio Spurs kwa pointi 94-90.
Taarifa zinaeleza kuwa vurugu zilitawala katika mitaa ya Times Square, ambapo mashabiki wa Knicks walichoma pia mabasi ya shule.
Ifahamike kuwa Knicks wametwaa ubingwa wao wa kwanza wa Ligi ya NBA baada ya kusubiri kwa miaka 53.


