17.4 C
New York

Ibrahimovic: Haaland? Hajafikia uwezo wangu

Published:

NEW YORK, Marekani

MKONGWE wa timu ya soka ya Taifa ya Sweden, Zlatan Ibrahimovic, amejitaja kuwa mshambuliaji bora kuliko Erling Haaland wa Manchester City.

Akihojiwa na kituo cha televisheni cha Fox Sports, Ibrahimovic aliyewahi kucheza kwa mafanikio makubwa AC Milan na PSG, amejiita straika aliyekamilika zaidi kuliko Haaland.

“Niliwahi kuaikia mahojiano yake akisema ndoto yake awapo uwanjani ni kugusa mpira mara mbili na kufunga mabao mawili. Kwangu, ndoto ilikuwa ni kugusa mpira mara mbili na kufunga mabao matatu,” amesema.

Hata hivyo, Ibrahimovic amemtaja Haaland kuwa ni mchezaji hatari zaidi ndani ya boksi, ukilinganisha na mastraika waliopo sasa.

Ibrahimovic anafahamika kwa kauli zake tata, akikumbukwa alivyowahi kusema hajawahi kutokea straika wa kufikia daraja lake katika ulimwengu wa soka.

Related articles

Recent articles