21 C
New York

Miaka 60 ya Uhuru| Tanzania ilivyosukwa

Published:

DESEMBA 9 kila mwaka, ni kumbukizi ya uhuru wa Tanzania kutoka kwa Waingereza na kwa mwaka huu itakuwa ni miaka 60 tangu ilipojitoa kwenye minyororo ya Wakoloni hao.

Tayari maandalizi ya kuelekea kwenye kilele cha Siku ya Uhuru yameanza, ikiwa ni pamoja na Serikali kupitia wizara na taasisi zake mbalimbali kuainisha mafanikio yaliyopatikana hadi sasa katika nyanja tofauti tofauti.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mohamed Mchengerwa, amekuwa wa kwanza kukutana na waandishi wa habari Makao Makuu ya nchi jijini Dodoma na kuelezea mafanikio mbalimbali, zikiwamo hatua muhimu zilizochukuliwa na awamu mbalimbali za Serikali katika kuhakikisha kuwa Tanzania inafika hapa ilipo.

Kwa mujibu wa Waziri Mchengerwa, mafanikio makubwa yameonekana ndani ya Tanzania kwa kuongezeka kwa ajira katika utumishi wa umma kutoka watumishi 17,566 mwaka 1961 hadi 528,290 mwezi Ocktoba, 2021.

Kati ya watumishi hao, wale wa sekta ya afya wamefikia 72,961, sawa na asilimia 13.8, wakati waalimu sasa ni 281,729, sawa na asilimia 53.3.

Aidha, Mchengerwa amesema katika kipindi cha miaka 60 ya Uhuru, Utumishi wa Umma umeendelea kuwa uliotukuka katika kuchagiza ustawi wa Taifa.

“Ni ngumu kutambua na kuthamini hatua kubwa tuliyopiga kama taifa katika kujijengea uwezo wetu wa kukabiliana na changamoto mbalimbali kwa kuendeleza taaluma mbalimbali ndani ya miaka 60 bila kujua tulikotoka,” amebainisha Mchengerwa.

Kupitia hotuba iliyowasilishwa na Waziri Mchengerwa, tovuti ya Gazetini imefanya uchambuzi wake kwa njia ya usanifu, ambao unaweza kuangalia hapo juu namna Tanzania ilivyosukwa au kuundwa hadi kufikia hapa ilipo.

[googlemaps https://www.google.com/maps?q=DODOMA&output=embed&hl=en-US&z=12&w=425&h=350]

Aidha, huu ni mwendelezo wa Gazetini kuchambua mambo makubwa yaliyotekelezwa na Serikali kwenye nyanja tofauti.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img