15.6 C
New York

Rodrygo afunguka magumu anayopitia

Published:

MADRID, Hispania

MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Rodrygo Goes, amepata majeraha ya goti yatakayomweka nje ya dimba kwa miezi isiyopungua 10.

Rodrygo alipata majeraha hayo katika mechi dhidi ya Getafe, ambayo Madrid walikuwa nyumbani Santiago Bernabeu na kufungwa bao 1-0.

Akitokea benchi na kushindwa kumaliza dakika 45 za kipindi cha pili, iilikuwa ni mechi ya kwanza kwa Mbrazil huyo tangu alipopona majeraha ya misuli.

Kwa majeraha hayo ya goti la mguu wa kulia, si tu atakosa mechi zote za Madrid zilizobaki msimu huu, bali pia hatoshiriki fainali za Kombe la Dunia zitakazoanza Juni, 2026.

“Moja ya siku mbaya zaidi katika maisha yangu. Nilikuwa nahofia sana kupata majeraha ya aina hii. Wakati mwingine, nahisi maisha yamekuwa na ukatili kwangu, lakini ni mara nyingi nimepata mafanikio nisiyotarajia,” amesema.

Rodrygo amefunga mabao matatu na kutoa ‘asisti’ sita katika mechi 27 alizocheza msimu huu wa 2025-26.

“Nitakuwa nje msimu mzima na kushindwa kuitumikia klabu yangu na nitakosa Kombe la Dunia kwa nchi yangu … Hakuna asiyejua ilivyo na maana kubwa kwangu,” amesema.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img