PRETORIA, Afrika Kusini
VIGOGO wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini, Kaizer Chiefs, imeanza tena kuifuatilia saini ya mlinda mlango wa timu ya taifa ya Nigeria ‘Super Eagles’, Stanley Nwabali.
Nwabali hana timu kwa sasa tangu alipoachana na Chippa United. Mtandao wa Afrik-Foot umeripoti kuwa Chiefs wanamuhitaji.
Awali, Chiefs walijaribu kumsajili kipa huyo baada ya kiwango bora alichokionesha katika fainali za AFCON 2023 zilizofanyika Ivory Coast.
Nwabali mwenye umri wa miaka 29, aliondoka Chippa United akiwa amecheza mechi 66 za Ligi Kuu ya Afrika Kusini.
Wachambuzi wa soka wanamtaja Nwabali kuwa mmoja ya makipa bora zaidi kuwahi kutokea katika historia ya Ligi Kuu hiyo.


