15.6 C
New York

Sakata la Bruno, Man United limekaaje?

Published:

MANCHESTER, Uingereza

KIUNGO wa Manchester United raia wa Ureno, Bruno Fernandes, hajaeleweka juu ya hatima yake klabuni hapo. Ataondoka au atabaki? Haijajulikana.

Bruno amekuwa mchezaji muhimu kwa Man United, ikiwamo msimu huu ambapo amefunga na bao saba na kutoa ‘asisti’ 14 katika mechi 27 za mashindano mbalimbali.

Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vya habari zinaeleza kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 31 anataka kuondoka Old Trafford mwishoni mwa msimu huu.

Wakati wa usajili wa kiangazi, 2025, hali ilikuwa hivi pia, ingawa alibaki Man United, licha ya klabu tajiri za Saudi Arabia kumtangazia dau nono.

Mkataba wake wa sasa utafikia ukomo Juni, 2027, hivyo endapo Man United watagoma kumuuza mwishoni mwa msimu huu, basi kuna hatari ya kuondoka akiwa mchezaji huru.

Man United, kwa upande wao, wanajaribu kumbakiza, ikielezwa kuwa tayari wamemwekea mezani ofa nono ili kumshawishi asaini mkataba mpya.

Gazeti la Mirror la Uingereza limeripoti kuwa mabosi wa Man United wako tayari kumlipa mshahara wa Pauni 400,000 kwa wiki endapo atabaki.

Hata hivyo, inasemekana Bruno amewapa masharti matatu ili amwage wino wa kumbakiza jijini Manchester.

Mosi, timu hiyo inapaswa kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Pili, anataka kujua kocha mpya. Tatu, anataka kujua usajili utakaofanyika ili kuimarisha kikosi.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img