MERSEYSIDE, Uingereza
LICHA ya mashabiki wa Liverpool kutokuridhishwa na mambo yanavyokwenda msimu huu, uongozi wa timu hiyo hauna mpango wa kumfuta kazi kocha Arne Slot.
Ukiwa ni msimu wake wa pili Anfield baada ya kuipa Liverpool taji la Ligi Kuu, safari hii Slot raia wa Uholanzi anapitia kipindi kigumu.
Kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa Manchester United wikiendi iliyopita kimeiacha Liverpool katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi, wakiwa wameachwa pointi 18 na vinara Arsenal.
Aidha, taarifa kutoka Uholanzi zinaeleza kuwa klabu ya Ajax inajaribu kumrejesha klabuni hapo kocha wake huyo wa zamani.
Kwa sasa, Slot ana mkataba na Liverpool, ambao unatarajiwa kufikia ukomo wake mwaka 2027.
Katika hatua nyingine, kiungo wa zamani wa Liverpool, Dietmarr Hamann, amesema: “Nimesikia kwamba Arne Slot atakuwa pale (Anfield) msimu ujao.”


