LONDON, Uingereza
GAZETI la Bild la Ujerumani limeripoti kuwa mabosi wa klabu ya PSG wanaweza kulitikisa soko la usajili duniani kwa kumchukua straika wa Bayern Munich, Harry Kane.
Bild limeeleza kuwa PSG wanaangalia uwezekano wa kukamilisha dili hilo kupitia dirisha kubwa la usajili, mwishoni mwa msimu huu.
Mkataba wa Kane na Bayern utafikia ukomo mwaka 2027, ingawa amesisitiza mara kadhaa nia yake ya kubaki klabuni hapo.
Bayern, kwa upande wao, wako mbioni kukaa mezani na straika huyo ili kujadili ishu ya mkataba mpya.
Awali, Real Madrid nayo ilitajwa kuwa kwenye mipango ya kumsajili nahodha huyo wa timu ya taifa ya England.


