LONDON, Uingereza
ARSENAL wanaangalia uwezekano wa kuanza na mshambuliaji wa Barcelona, Dani Olmo, pindi tu dirisha kubwa la usajili la kiangazi litakapofunguliwa.
Ripoti zinaeleza kuwa Arsenal wamefanya mazungumzo na Barcelona, wakijaribu kuulizia upatikanaji wa nyota huyo.
Olmo (27), hana uhakika wa namba katika kikosi cha kocha Hansi Flick na msimu huu amecheza mechi 23 pekee, tena 16 akitokea benchi.
Licha ya mechi chache za La Liga alizopata nafasi ya kucheza, nyota huyo amefunga mabao saba na kutoa ‘asisti’ saba.
Barcelona, kwa upande wao, hawana mpango wa kumuuza, na hata Olmo naye anataka kubaki Camp Nou na kupambania namba yake kikosini.


