MANCHESTER, Uingereza
MANCHESTER United imetenga kitita cha Pauni milioni 39 ili kufanikisha usajili wa kiungo wa Villarreal, Pape Gueye.
Gueye amekuwa na msimu mzuri, ambapo amefunga mabao manne na kutoa ‘asisti’ mbili katika mechi 32 za mashindano mbalimbali.
Kwa La Liga, nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 amefunga mabao manne na asisti mbili. Amecheza mechi sana za Ligi ya Mabingwa.
Mkataba wake na Villarreal utafikia ukomo mwaka 2028 lakini una kipengele kinachomruhusu kuondoka kwa Pauni milioni 39.
Mabosi wa Man United wako tayari kulipa kiasi hicho cha fedha ili kiungo huyo awe Old Trafford msimu ujao.


