6.5 C
New York

Afrika na chanjo ya bei nafuu ya Ukimwi

Published:

KAMPALA, Uganda

UGANDA itapokea mzigo wake wa kwanza wa dawa za chanjo ya Ukimwi ya Lenacapavir baada ya kuwasili nchini Zambia jana Novemba 25, 2026.

Dawa hizo ni kinga ya sindano ya mara mbili kwa mwaka, ikielezwa kuzuia maambukizi kwa asilimia takribani 100.

Matumaini mapya kwa Afrika ni bei nafuu ya dawa hizo, ambazo zitagharimu Dola 40 tu kwa mtu mmoja kupata chanzo ya mwaka mmoja.

Zimbabwe inatarajiwa kupokea mzigo wa dawa hizo mapema mwaka 2027, zikitarajiwa pia kuzifikia nchi zingine za Afrika.

Aidha, dawa hizo zinazalishwa na kusambazwa na kampuni ya Gilead Sciences ya nchini Marekani.

Hata hivyo, hizi ni za daraja la pili kwani zile ‘original ni gharama Zaidi, zikitajwa kugharimu mtu mmoja Dola 28,000 kwa mwaka.

Lenacapavir zina sifa ya kuharibu mfumo wa virusi vya Ukimwi kujizalisha na kusababisha maambukizi ndani ya mwili.

Kabla ya kuletwa Afrika, tayari ilifanyika kliniki ya majaribio iliyohusisha vijana wa kike na wa kiume zaidi ya 5,000 wa Uganda na Afrika Kusini mwaka 2024.

Afrika Kusini inatajwa kuwa moja ya nchi zenye kiwango kikubwa cha maambukizi ya Ukimwi si tu barani Afrika, bali ulimwenguni kwa ujumla.

Kwa mujibu wa takwimu za Taasi ya Global Fund, watu zaidi ya 189,000 duniani kote wameshapata chanjo ya Lenacapavir.

Wakati huo huo, Global Fund wanatarajia chanjo hiyo kuzifikia nchi 24 kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Kwa takwimu za Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa [WHO], watu milioni 41 wanaishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi duniani. Kwa mwaka jana pekee, ugonjwa huo uliua watu 570,000.

Related articles

Recent articles