LOS ANGELES, Marekani
MFUNGWA wa kike aliyekuwa mjamzito ametoroka wakati akirudishwa gerezani baada ya kutoka kwenye matibabu.
Rebecca Taylor [26], alinufaika na kitendo cha polisi waliokuwa wakimsafirisha kushuka kwenye gari na kwenda kununua chakula, ikielezwa kuwa bibiye huyo aliendesha na kutokomea.
Hata hivyo, mamlaka za gereza zimeeleza kuwa Taylor hajakamatwa lakini nguo zake na gari hilo la wagonjwa [ambulance] vilikuja kuonekana baadaye.
Bibiye huyo alikuwa rumande kwa kesi kadhaa za wizi, kwa mujibu wa taarifa ya mamlaka za gereza.
Kwa upande mwingine, vyanzo vya habari vimeeleza kuwa Taylor hakuwa peke yake kwenye gari hilo, bali alitoroka na mwenzake.


