18.2 C
New York

Koffi Olomide: Kesi ya madansa wake, kumdunda mwandishi – [5]

Published:

KINSHASA, DRC

ILIKUWA Februari 13, 2012, ambapo Koffi alifikishwa mahakamani jijini Paris, Ufaransa, baada ya kufungiliwa mashitaka na madansa watatu aliowahi kuwaajiri katika Bendi ya Quartier Latin International kuanzia mwaka 2006 hadi 2008.

Madansa hao, akiwamo mmoja wa umri chini ya miaka 18, walidai kuwa staa huyo aliwadhalilisha kingono, ikiwamo kuwafungiwa ndani kama mateka kwenye moja ya nyumba zake jijini Paris.

Mabinti hao waliieleza mahakama kuwa Koffi aliwachukua kutoka DRC na kuwaingiza kinyemela nchini Ufaransa. Kesi ilidumu kwa miaka takribani mitano na hatimaye Kofi alihukumiwa kifungo cha nje cha miezi 18, pamoja na kutakiwa kulipa faini.

Mwaka huo pia, Koffi alikamatwa na polisi akiwa studio mjini Kinshasa na kushitakiwa kwa kumpiga prodyuza wake, Diego Music Lubaki, lakini baadaye mlalamikaji aliamua kufuta kesi hiyo.

Ni mwaka huo huo, Koffi akiwa Rwanda alimdhalilisha kwa kumpiga usoni mwandishi wa habari, Jean Nepomuscene Ndayisenga, wakati akijaribu kumpiga picha baada ya kumaliza shoo.

Licha ya Koffi kuomba radhi, Ndayisenga alifungua keshi akisema kipigo hicho kilisababisha avunjike kidole, pamoja na kamera yake kuharibika. Kesi ilizimwa baada ya kukosekana kwa ushahidi.

Mwaka 2016, Koffi akitarajiwa kutumbuiza mjini Nairobi, Kenya, lakini shoo hiyo haikufanyika kwani staa huyo alikamatwa na polisi kwa tukio lake la kumpiga mateke ya tumbo dansa wake, Pamela, muda mfupi tu baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta.

Mwaka 2018, sekeseke la mwandishi wa Rwanda, Ndayisenga, ‘lilifufuka’ baada ya Koffi kuwasili Zambia kwa ajili ya shoo. Alitaka msanii huyo akamatwe na polisi wa Zambia, ombi ambalo hata hivyo halikukubaliwa na mamlaka za nchi hiyo.

Miezi michache baadaye, Mahakama nchini Ufaransa ilimkuta na hatia katika kesi ya kumbaka mmoja ya madansa wake aliyekuwa na umri wa miaka 15 wakati huo. Alihukumiwa kifungo cha nje cha miaka miwili.

Itaendelea …

Related articles

Recent articles