18.1 C
New York

Waziri wa Saudia awalaani Houthi

Published:

RIYADH, Saudi Arabia

WAZIRI wa Nishati wa Saudi Arabia, Abdul Aziz bin Salman, amelaani mashambulizi yaliyofanywa na wapiganaji wa Kundi la Houthi la Yemen.

Houthi wanaishambulia Saudia kwa kuwa nchi hiyo imekuwa ikiiunga mkono serikali iliyoko madarani nchini Yemen.

Kundi hilo limetekeleza mashambulizi kadhaakatika viwanja vya ndege na vituo vya mafuta na gesi nchini Saudi Arabia.

“Mashambulizi ya wiki za hivi karibuni ni makali zaidi. Hata majibu yetu [dhidi ya Houthi] yanapaswa kuwa makali pia,” amesema Bin Salman.

“Sisi kama Saudia hatuhofii, ni watu makini. Tutaithibitishia dunia kwamba tutalipiza kwa kila tunachofanyiwa.”

Wikiendi iliyopita, mwanaume raia wa Pakistan aliuawa katika shambulizi la Mfalme wa Kimataifa wa Khalid.

Shambulizi hilo lilikuja ikiwa ni siku moja tu tangu Houthi waliposhambulia kiwanja kingine cha ndege na kusababisha vifo 13.

Related articles

Recent articles