12.7 C
New York

Ronaldo apigwa ‘stop’ Ureno

Published:

PPORTUGAL, Ureno

SHIRIKISHO la Soka la Ureno (FPF) limemwekea nahodha wa timu ya taifa, Cristiano Ronaldo, adhabu ya kusimamishwa kwa muda kufuatia kuondoka kwake kambini mwezi Septemba, katika tukio lililozua mvutano ndani ya timu hiyo.

Ronaldo, mwenye umri wa miaka 41, alijiondoa kwenye kikosi cha Ureno kilichokuwa kikijiandaa kwa mechi za Ligi ya Mataifa, baada ya kuachwa nje ya kikosi kilichocheza dhidi ya Norway na kubaini kuwa hakuwa akitarajiwa kuanza mechi dhidi ya Denmark.

Mshambuliaji huyo wa klabu ya Al-Nassr baadaye alitoa taarifa akieleza kuwa aliondoka kutokana na kile alichodai kuwa ni kuvunjwa kwa ahadi mara mbili na kocha wa Ureno, Jorge Jesus, akieleza kuwa hatua hiyo ilivunja uaminifu kati yao.

Katika taarifa yake, FPF ilisema kuwa ilimwekea Ronaldo kizuizi cha muda Oktoba 9, huku suala hilo likiainishwa kuwa la dharura.

Kwa mujibu wa kanuni za FPF, mchezaji anayeshindwa kuripoti au kuondoka kwenye majukumu ya timu ya taifa anaweza kukabiliwa na adhabu ya kusimamishwa kwa kipindi cha mwezi mmoja hadi sita, pamoja na faini ya fedha.

Hata hivyo, Rais wa FPF, Pedro Proença, amesema kuna haja ya kutuliza hali huku taratibu za kinidhamu zikiendelea.

Akizungumza na gazeti la Ureno la Record, Proença alisema pande husika zimekaa mezani na kuna nia ya kumrejesha Ronaldo katika kikosi cha taifa. Alisisitiza kuwa suala hilo litashughulikiwa kupitia mchakato wa kawaida wa kinidhamu.

Related articles

Recent articles