Na mwandishi wetu, Gazetini
SIKU chache zilizopita, Eritrea ilitangaza kusitisha uhusiano wake wa kidiplomasia na majirani za, Ethiopia, ikiwa ni hatua kubwa Zaidi katika mgogoro wa muda mrefu wa Ardhi kati ya nchi hizo.
Aidha, hatua hiyo inakuja wakati huu kukiwa na mapigano makali Kaskazini mwa Ethiopia kati ya Serikali na wapiganaji wa Tigray People’s Liberation Front (TPLF).
Serikali ya Adis Aaba inaamini kuwa Eritrea imekuwa ikiwapa nguvu maadui zake hao. Ethiopia imekuwa kwenye hali mbaya ya kiusalama tangu nchi hiyo ilipotoka katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka miwili [2020 – 2022].
HISTORIA YA UADUI WA ERITREA, ETHIOPIA
Uhusiano kati ya nchi jirani zimekuwa na uadui kwa miaka mingi. Mwaka 1962, Ethiopia iliivamia Eritrea. Baada ya mapigano, hatimaye Rais wa sasa, Isaias Afwerki, aliiongoza Eritrea kupata uhuru mwaka 1993.
Nchi hizo ziliingia tena kwenye vita ya kuwania mipaka kuanzia mwaka 1998 hadi 2000. Waziri Mkuu, Abiy Ahmed, alipoingia madarakani mwaka 2018, alijaribu kujenga uhusiano wa kidiplomasia na Eritrea.
Hata hivyo, wakati Ethiopia ilipoingia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe kuanzia mwaka 2020 hadi 2022, Eritrea iliripotiwa kuwasaidia wapiganaji wa Tigray [TPLF].
Hivi karibuni, Ethiopia ilifunga ofisi za ubalozi wake mjini Asmara, Eritrea, pamoja na kuwatimua wanadiplomasia 10 wa nchi hiyo.
Mbali na Eritrea, pia Ethiopia inazishutumu Misri na Sudan kuwasaidia waaasi wa Tigrayan, hali inayotishia uhusiano wake na mataifa mawili hayo.
MISRI, ETHIOPIA NAZO HAZIIVI
Kwa muda mrefu sasa, Ethiopia na Misri zimekuwa ‘chui na paka’. Chanzo ni mradi wa Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance Dam (GERD) ambao Misri inaulalamika kwa madai kuwa unatishia usalama wa vyanzo vyake vya maji.
Hivi karibuni, Misri iliwaagiza wanadiplomasia wa Ethiopia kuondoka nchini humo. Hatua hiyo ilikuja baada ya Ethiopia kuwatimua wanadiplomasia wa Misri.
Wakati huo huo, Sudan inaelekeza lawama zake kwa Ethiopia ikidai kuwa nchi hiyo inafadhili waasi. Ethiopia imekanusha mara zote shutuma hizo.


