LONDON, Uingereza
WAANDAAJI wa Ballon d’Or wamefichua nchi za Afrika zilizompigia kura Harry Kane kutwaa tuzo hiyo kwa mwaka huu.
Pia, waandaaji hao ambao ni jarida la France Football, wamefichua nchi za Afrika zilizomchagua Kylian Mbappe na Lamine Yamal katika kinyang’anyiro hicho.
Kwa mujibu wa utaratibu wa kupata mshindi, waandishi wa habari, wakiwamo wa Afrika, hupata nafasi ya kupiga kura.
Sasa, kwa mujibu wa France Football, waandishi wa nchi za Senegal, Angola, Afrika Kusini na Uganda walimpigia kura Kane.
Aidha, waandishi wa nchi tisa za Afrika walipeleka kura zao kwa nahodha wa timu ya soka ya Taifa ya Ufaransa, Mbappe.
Nchi hizo ni Benin, Cameroon, Ivory Coast, Misri, Ghana, Guinea, Mali, DR Congo na Zambia.
Kwa upande wake, Yamal alivuna kura kutoka kwa mataifa ya Cape Verde, Burkina Faso, Algeria na Tunisia.
Lakini, hakuna kati ya Kane, Mbappe na Yamal aliyepata kura kutoka Nigeria, na badala yake nchi hiyo ilimchagua kiungo wa Barcelona, Rodri.


