LONDON, Uingereza
KLABU ya Arsenal imetenga kiasi cha Pauni milioni 33 ili kufanikisha usajili wa kinda wa Kibrazil, Eduardo Pape.
Akiwa na umri mdogo tu wa miaka 17, Pape amekuwa mchezaji muhimu kwenye U-20 ya klabu ya Cruzeiro ya Ligi Kuu nchini Brazil.
Akiwa na kikosi hicho, ameshacheza mechi 32, akihusika katika mabao sita, akifunga matatu na kutoa ‘asisti’ tatu.
Katika mechi nane za hivi karibuni, Pape amefunga mabao sita na anatarajiwa kuwa sehemu ya U-17 ya Brazil katika fainali zijazo za Kombe la Dunia la vijana.
Hata hivyo, vyanzo vya habari nchini Brazil vimedai kuwa mkataba wake utakwisha mwaka 2029 na huenda akaongeza miaka mingine mitatu ya kukomaa zaidi.


