23.2 C
New York

Uchaguzi Mkuu Israel: Netanyahu dhidi ya vyama vya Kiarabu

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

HIVI karibuni, Mahakama Kuu nchini Israel ilipitisha uamuzi wa kuviruhusu vyama vya upinzani vya Kiarabu kushiriki Uchaguzi wa Wabunge unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.

Awali, Kamati ya Uchaguzi [CEC] iliviwekea zuio yyama vine vya Kiarabu. Hatua hiyo iliambatana na kuwapiga kufuli baadhi ya wagombea.

Ni kwa maaana hiyo, sasa United Arab List, maarufu kwa jina la Ra’am, na muungano wa Hadash, Balad na Ta’al vitashiriki Uchaguzi huo wa Oktoba 27, 2026.

Kwa upande mwingine, Mahakama ilitengua uamuzi wa CEC kumtoa kwenye kinyang’anyiro mgombea wa kiti cha Ubunge wa Chama cha Hadash, Ofer Cassif.

Hatua hiyo ilienda sambamba na ushauri wa Mahakama kwa kiongpozi wa Chama cha Kipalestina cha Balad, Sami Abu Shehadeh, kujiondoa kwa hiari kwenye kinyang;anyiro cha kuwania ubunge.

Kamati Kuu hiyo, CEC, ina mkono wa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu. Madai ni kwamba vyama hivyo vimekuwa vikiunga mkono vikundi vya kigaidi.

Baadhi ya vyama, kikiwamo Likud cha Netanyahu, vilipaza sauti vikitaka vyama vya Kiarabu na baadhi ya wagombea kuondoshwa kwenye mbio za Uchaguzi.

Related articles

Recent articles