21.3 C
New York

Simba yatamba ugenini, Wamalawi hawaamini!

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

SIMBA imeuanza vizuri msimu huu wa Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuinyuka Mighty Wanderers bao 1-0 katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Kimataifa wa Bingu mjini Lilongwe.

Katika mchezo huo wa hatua ya awali, ‘Wekundu wa Msimbazi’ walipata bao pekee hilo dakika ya 66, mfungaji akiwa ni nyota wake raia wa Ivory Coast, Anicet Oura.

Kituo kinachofuata kwa Wekundu wa Msimbazi ni Ligi Kuu Bara, ambapo watashuka dimbani Septemba 9, 2026, kwa mechi yao dhidi ya matajiri wa Chamazi, Azam FC.

Baada ya mechi hiyo, Simba watakuwa na siku chache za kuisubiri Mighty Wanderers kwa ajili ya mchezo wa marudiano.

Ifahamike kuwa mshindi wa jumla kwa matokeo ya mechi mbili atakwaana na aidha 15 de Agosto ya Guinea ya Ikweta au Fomboni FC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Comoro.

Related articles

Recent articles