21.3 C
New York

Andy Ruiz arejea kwa kichapo ulingoni

Published:

LOS ANGELES, Marekani

ALIYEWAHI kuwa bingwa wa dunia kwa ngumi za uzito wa juu, Andy Ruiz Jr, amepoteza pambano lake la kwanza tangu alipopona majeraha.

Andy Ruiz amepigwa na bondia wa kimataifa wa Poland, Damian Knyba, katika pambano lililopigwa mjini New Jersey, Marekani.

Katika pambano dhidi ya Knyba, majaji wote watatu walimpa mpinzani wake huyo ushindi wa pointi 117-110, 114-113 na 114-113.

Bondia huyo mwenye umri wa miaka 36, alipata jina kubwa miaka saba iliyopita alipoishangaza dunia kwa kumdunda Anthony Joshua.

Kwa muda saa, Andy Ruiz amekuwa akisumbuliwa na majeraja na pambano dhidi ya Knyba lilikuwa la kwanza tangu Agosti, 2024, ambapo alipata sare mbele ya Jarrell Miller.

Akizungumza baada ya kupoteza, Andy Ruiz amesema licha ya muda mrefu aliokaa nje ya ulingo, hakutaka mpinzani mwepesi na ndiyo maana alimchagua Knyba.

“Sikutaka pambano jepesi, kwa hiyo ndiyo maana nilimchagua Damian. Ni mkubwa. Bado nipo na nataka kuendelea kupigana,” amesisitiza.

Related articles

Recent articles