22.1 C
New York

Ferdinand ataja usajili bora England

Published:

LONDON, Uingereza

NAHODHA wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand, amesema usajili bora wa kipindi hiki cha kiangazi ni ule wa winga mpya wa Arsenal, Christos Tzolis.

Tzolis alisajiliwa na Arsenal kwa ada ya Pauni milioni 34 akitokea Club Brugge ya Ligi Kuu nchini Ubelgiji.

Nyota huyo wa kimataifa wa Ugiriki ameonesha uwezo mkubwa katika mechi alizocheza, licha ya kwamba bado hajafunga bao.

“Arsenal hawajasajili sana lakini nafikiri wamekuwa na mipango mizuri kwa namna walivyokwenda na usajili wao,” amesema.

Katika hatua nyingine, Ferdinand aliyewahi pia kuwa beki tegemeo wa timu ya soka ya Taifa ya England, amesema mashabiki wa Arsenal wasubiri makubwa kutoka kwa mchezaji huyo.

Related articles

Recent articles