MIAMI, Marekani
BAADA ya Lionel Messi kutangaza kustaafu kuitumikia timu ya Taifa ya Argentina, beki wa kikosi hicho, Rodrigo De Paul, ameibuka na ujumbe wa kumuaga.
Mshambuliaji huyo alianza kuitumikia Argentina mwaka 2005, wakati huo akiwa na umri wa miaka 18. Ameifungia mabao 125 na asisti 68 katika mechi 207.
De Paul anayecheza naye katika klabu ya Inter Miami ya Marekani, amemshukuru Messi kwa mchango wake wakiwa kwenye kikosi cha timu ya taifa.
Hivi karibuni, winga wa zamani wa Argentina, Angel Di Maria, alimshukuru Messi kwa kulichagua Taifa hilo, licha ya kwamba angeweza kucheza Hispania, Italia au Brazil.
Kwa upande wake, De Paul alisema Messi atakumbukwa si tu kwa uwezo, bali pia kwa uongozi wake ndani ya uwanja.
“Ninachoweza kufanya ni kukuaga tu. Wewe ni mchezaji bora zaidi katika historia. Asante kwa kutupa furaha …” amesema De Paul.


