RIYADH, Ureno
KLABU ya Al Hilal imethibitisha kuachana rasmi na straika wake raia wa Ufaransa, Karim Benzema, ikieleza kuwa ni makubaliano ya pande mbili.
Benzema aliyewahi kucheza Lyon na Real Madrid, ana umri wa miaka 38 na anaondoka klabuni hapo baada ya miezi sita tu tangu aliposajiliwa.
“Klabu ya Al Hilal na mchezaji raia wa Ufaransa, Karim Benzema, wamefikia hatua ya kuvunja mkataba kwa makubaliano ya pande mbili na kuhitimisha utumishi wake katika timu,” imeeleza taarifa ya klabu hiyo.
Kuondoka kwa Benzema linakuja muda mfupi baada ya Al Hilal kukamilisha usajili wa straika kutoka Aston Villa ya England, Ollie Watkins.
Wakati huo huo, Benzema ametimka klabuni hapo, licha ya kwamba amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake.


