26.5 C
New York

Ukweli uliojificha kuhusu uwezo wa kijeshi wa Iran

Published:

TEHRAN, Iran

JESHI la Mapinduzi ya Kiislam la Iran (IRGC) limejipanga kujibu mapigo kwa Marekani iliyotangaza ‘kiama cha uchumi’ kwa nchi hiyo ya Mashariki ya Kati.

Marekani imeweka wazi kuwa inataka kuangusha uchumi wa Iran kwa kuziwekea vikwazo, ikiwamo kuzinyima misaada, nchi zote zinazofanya nayo biashara.

Rais wa Marekani, Donald Trump, ameiita hatua yao hiyo kuwa ni ‘operesheni kali zaidi ya kiuchumi’ kuwahi kuifanya dhidi ya Serikali ya Iran.

Hata hivyo, makamanda wa jeshi la Iran wao wanajipanga na mikakati ya kivita, lengo likiwa ni kuifanya Marekani ijutie hicho inachokifanya.

Mkuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wa Iran, Ali Abdollahi, amesema kwa sasa wanajivunia mapinduzi makubwa ya uzalishaji wa ndani wa silaha.

Kwa upande wake, Msemaji wa Wizara ya Ulinzi, Reza Talaei-Nik, amesema uamuzi wa kusitisha kufanya maonesho ya silaha zao mpya umelenga kuwapa ‘surprise’ maadui zao ndani ya uwanja wa vita.

Lakini, kwa mujibu wake, Iran imezidisha zaidi ya mara tatu kiwango cha uzalishaji wa silaha na teknolojia tangu vita vyao na Marekani vilipoanza Februari 28, 2026.

Talaei-Nik aliongeza kuwa kampuni zaidi ya 9,300 nchini Iran zinajihusisha na uzalishaji wa silaha, hivyo ni ngumu kwa Marekani na Israel kuiangusha sekta hiyo.

Naibu Waziri wa Ulinzi, Majid Ebn-e Reza, alisisitiza kuwa Iran kwa sasa imeimarisha uwezo wake wa kupenya na kuingia kwenye kambi za maadui, usahihi wa kushambulia maeneo yaliyolengwa, na kutibua mashambulizi ya anga.

Kwa maana nyingine, ni tofauti na madai ya Marekani, kwamba imesambaratisha asilimia zaidi ya 85 ya sekta ya ulinzi ya Iran, zikiwamo ndege zisizo na rubani za masafa marefu.

Wakati huo huo, ni tofauti na madai ya awali ya Marekani, kwamba imesambaratisha meli za kivita zaidi ya 150 za Iran.

Makamanda wa jeshi la Iran wamedai kuwa tangu waliposhambuliwa Julai, 2026, wamekuja na mkakati mpya wa kuanzisha kambi na viwanda vya utengenezaji wa silaha vya chini ya ardhi katika maeneo ya Kusini ya nchi hiyo.

Aidha, mbali na zile nzito, Iran wanajivunia silaha na teknolojia nyepesi, zikiwamo ‘drone’, ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikitumika kuishambulia na hata kutibua mashambulizi ya Marekani na Iran.

Vyombo vya habari vya Marekani vinakiri kuwa ndege zake za kivita zenye thamani ya zaidi ya Dola bilioni 1.3 zimedunguliwa au kupotezwa hewani na Iran.

Related articles

Recent articles