LAGOS, Nigeria
KAMPENI kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Januari, 2027, zilianza wiki hii nchini Nigeria. Rais aliyeingia madarakani mwaka 2023, Bola Tinubu, anagombea muhula wake wa pili madarakani.
Changamoto ni zile zile; uhaba wa ajira kwa vijana, umasikini, ubovu wa miundombinu, pamoja na hali mbaya ya usalama katika nchi hiyo inayoongoza kwa idadi kubwa ya watu barani Afrika.
Kuelekea Uchaguzi ujao wa Januari 16, tafiti zinaonesha kuwa asilimia takribani 80 ya raia wa Nigeria hawaamini kuwa nchi yao iko kwenye mwelekeo sahihi.
Kati yao, asilimia 45 wanalalamikia ugumu wa maisha na hali isiyoridhisha ya usalama, kwa mujibu wa utafiti wa Shirika la SBM Intelligence.
Tinubu aliyeingia madarakani mwaka 2023 anakabiliwa na upinzani kutoka kwa wagombea wengine 18 wa kiti cha urais kupitia vyama vya upinzani.
Kwa upande mwingine, wachambuzi wa siasa wanaona Uchaguzi huo hauna tofauti kubwa na ule uliopita (2023) katika kinyang’anyiro cha urais.
Kama ilivyokuwa mwaka 2023, safari hii pia ni vigogo watatu wanaochuana vikali, ambao ni Tinubu, Makamu wa Rais wa zamani, Atiku Abubakar, na Gavana wa zamani, Peter Obi.
Katika Uchaguzi huo, Tinubu wa Chama cha All Progressives Congre (APC) aliwapiku akiwa na ushindi wa asilimia 36.6, akifuatiwa na Abubakar (29%) na Obi (25%).
Muhula wake wa kwanza madarakani umeshuhudia Benki ya Dunia (WB) ikiuaja uchumi wa Nigeria kukua kwa kasi, ingawa wananchi wake hilo likitafsiri uhalisi wa maisha yao ya kila siku.
Wapo waliompachika jina la ‘T-Pain’ kueleza maumivu wanayopitia kutokana na kupanda kwa gharama za bei ya vyakula, makazi na usafiri.
Mwandishi wa habari wa Gazeti la siasa la The Bellwether, Afolabi Adekaiyaoja, anasema hali mbaya ya kiuchumi inachangia hata hali mbaya ya usalama nchini humo: “Uchumi ndiyo tatizo kubwa zaidi,” anasisitiza.
Kuhusu hali ya usalama, mbali ya vikundi vya waasi vilivyoweka mizizi katika maeneo mengi, Boko Haram ni tatizo jingine, hasa Kaskazini mwa Nigeria.


