24.7 C
New York

Chama tawala kilichogeukia siasa za upinzani

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

WAKATI fulani, Peoples Democratic Party (PDP) kilikuwa Chama tawala nchini Nigeria. Chama kikongwe kilichoasisiwa mwaka 1998.

Kwa miaka 16, kabla ya kuangushwa katika Uchaguzi wa mwaka 2015, kiliunda Serikali chini ya marais watatu tofauti; Olusegun Obasanjo, Umaru Musa Yar’Adua na Goodluck Jonathan.

Si tu kushika nchi katika nafasi ya urais, pia ushawishi wa PDP ulikifanya Chama hicho kutawala sehemu kubwa ya majimbo 36 ya Nigeria.

Upepo ulibadilika ghafla mwaka 2015 baada ya wananchi kukipa kisogo na kumchagua mgombea wa urais wa Chama pinzani cha All Progressives Congress (APC), Muhammadu Buhari.

APC kilikuwa Chama kipya wakati huo, kikitokana na muungano wa vyama vya upinzani, pamoja na vigogo walioondoka ndani ya PDP.

Kikiwa Chama cha upinzani, PDP kilianza kupitia nyakati ngumu, hasa mwaka 2025, ambapo baadhi ya magavana wake walikimbia na kuhamia Chama tawala, APC.

Hadi kufikia Desemba, 2025, Chama hicho kilikuwa na majimbo matatu pekee baada ya magavana watano wa Delta, Akwa Ibom, Enugu, Bayelsa na Rivers kukihama Chama hicho.

Hali ilikuwa mbaya zaidi mwaka 2026, ambapo PDP ilipoteza majimbo matatu yaliyobaki, likiwamo la Oyo ambalo Gavana wake alihamia APC wiki chache zilizopita.

Kwa sasa, ikiwa imebaki miezi takribani mitano kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Januari, 2026, bado APC ndiyo inayounda Serikali chini ya Rais Bola Tinubu.

Je, kuna uwezekano wa PDP ‘kufufuka’? Mwanasiasa na mwanachama mkongwe mkongwe wa Chama hicho, Aminu Adamu, anaamini hilo linawezekana.

Anatolea mfano kilichotokea Thailand na Argentina, ambako vyama tawala vilipoteza nguvu na kuwa upinzani, kisha kujisahisisha na kurudi madarakani.

“Si jambo geni. Tumeona hilo likitokea. Tunachotakiwa ni kukaa pamoja na kujijenga upya. Kama tutajisahihisha, nafikiri PDP itakuwa imara zaidi mwaka 2032,” amesema Adamu.

Hata hivyo, kwa baadhi ya wachambuzi wa siasa, mwaka 2032 ni mapema mno kwa PDP kuwa imejijenga tena na kuwa na ushindani katika siasa za Nigeria.

Kwa upande wake, mchambuzi Deji Olarenwaju anaamini njia pekee ya PDP kurejesha nguvu yake ni kwa kuungana na vyama vingine vya upinzani.

Olarenwaju anavitaja African Democratic Congress (ADC) au Nigeria Democratic Congress (NDC), akisema: “Bila kufanya hivyo, haiwezekani kwa PDP kurudi yenyewe.”

Related articles

Recent articles