27.5 C
New York

Ligi Kuu ya Uturuki msimu ujao ni balaa zito

Published:

INSTANBUL, Uturuki

KAMA hujawahi kufuatilia Ligi Kuu ya Uturuki, basi hebu jaribu kufanya hivyo msimu ujao (2026-27) kwani kuna uhondo wa ‘kufa mtu’ kutokana na usajili uliofanyika majira haya ya kiangazi.

Galatasaray wanasaka taji lao la tano mfululizo lakini safari hii wana kazi kubwa ya kufanya ili kufanikisha malengo yao hayo.

Fenerbahce wametumia euro milioni 39 kuimarisha safu yao ya ushambuliaji kwa kumsajili Mason Greenwood kutoka Marseille.

Greenwood ametoka kufunga mabao 37 na asisti 13 katika mechi 66 za Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1).

Wakati huo huo, Fenerbahce imeinasa saini ya mshambuliaji tishio wa kimataifa wa Kosovo, Vedat Muriqi.

Muriqi ametua kikosini akitokea Real Mallorca aliyojiunga nayo msimu wa 2021-22 na ameondoka akiwa mfungaji bora wa muda wote klabuni hapo.

Nyota huyo alimaliza msimu uliopita (2025-26) akiwa nafasi ya pili kwenye chati ya wafungaji wa La Liga baada ya kuzifumania nyavu mara 23.

Kama hiyo haitoshi, mabosi wa klabu hiyo wameliongezea nguvu eneo la ulinzi kwa kumsajili beki kutoka Manchester City, Nathan Ake.

Mlinzi huyo wa kati wa kimataifa wa Uholanzi ameondoka Man City baada ya miaka sita ya mafanikio akiwa na matajiri hao wa Ligi Kuu ya England (EPL).

Besiktas nao wameimarisha kikosi chao kipindi hiki cha usajili wa kiangazi. Si tu ujio wa kiungo Orkun Kokco, bali pia wameinasa saini ya winga kutoka Arsenal, Leandro Trossard.

Kwa upande mwingine, Trabzonspor nao si wa kuwabeza, licha ya kumaliza msimu uliopita wakiwa nafasi ya nane kwenye msimamo wa Ligi.

Klabu hiyo imefanikiwa kuinasa huduma ya mshambuliaji tishio wa zamani wa Liverpool, Mohamed Salah. Ni baada ya staa huyo mwenye umri wa miaka 34 kukataa ofa nono za klabu za Saudi Arabia.

Related articles

Recent articles