28.6 C
New York

Haya ndiyo maajabu ya nchi iliyobadili jina

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

KWA miaka mingi, iliitwa Nauru, kabla ya kubadili jina hivi karibuni na kujiita Jamhuri ya Naoero. Inafahamika kuwa ni nchi ya tatu kwa udogo duniani, ikiwa na ukubwa wa kilometa za mraba 21 na watu 12,000 pekee.

Juni, 2026, Serikali ya Kisiwa hicho kilichopo katika Bahari ya Pacific ilipeleka ombi lake la kubadilisha jina kwa Umoja wa Mataifa, mchakato ambao pia ulipitia kura zilizopigwa na wabunge.

Wakati huu ikisherehekea jina jipya, Jamhuri ya Naoero iko hatarini kupotea kwani ardhi yake imekuwa ikizama taratibu baharini kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Hivyo, Machi, 2025, Serikali ilitangaza mpango wake wa hati ya kusafiria ya dhahabu (Golden Passport) ukilenga kuchangisha fedha za kuhamisha asilimia 90 ya watu wake na kuwapeleka maeneo ya juu zaidi.

Kwa udogo wake, Jamhuri ya Naoero inazidiwa na nchi mbili pekee, ambazo ni Tuvalu na Vatican. Nchi ya nne kwa udogo ni Palau iliyoko Magharibi mwa Bahari ya Pacific.

Naoero, wakati huo ikiwa Nauru, ilitawaliwa na Ujerumani, kisha kuwa chini ya Australia, kabla ya kujitangazia uhuru wake mwaka 1968.

Katika miaka ya 1970, Kisiwa hicho kilikuwa na utajiri mkubwa wa madini, lakini kiliporomoka na kusababisha hali mbaya ya kiuchumi miaka ya 1990.

Kama zilivyo nchi zote zisizo chini ya utawala wa kifalme, Naoero inaongozwa na rais, ambaye ni David Adeang, Makamu wake ni Lionel Aingimea, huku Spika wa Bunge akiwa Marcus Stephen.

Mbali na Umoja wa Mataifa, nchi hiyo ni mwanachama wa Jumuhiya ya Madola, Umoja wa nchi za Afrika, Caribbean na Pasific, Benki ya Maendeleo ya Asia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).

Kwa upande mwingine, haiwi nchi ya kwanza kubadili jina. Eswatini, ambayo awali ilifahamika kwa jina la Swaziland, ilifanya hivyo pia mwaka 2018.

Mfano mwingine ni mwaka 2022, ambapo Uturuki iliuandikia barua Umoja wa Mataifa ikiomba ifahamike kwa jina la ‘Türkiye’ badala ya ‘Turkey’.

Related articles

Recent articles