LAGOS, Nigeria
MWIGIZAJI maarufu wa filamu za Nigeria (Nollywood), Ruth Kadiri, amevunja ukimya baada ya taarifa za kifo chake kusambaa na kuzusha taharuki mitandaoni.
Kupitia mitandao, Kadiri amewahakikishia mashabiki wake wa kuwa yuko hai na ana afya nzuri, hivyo wasiwe na wasiwasi wala kupotoshwa na uvumi huo,” amesema.
Kuibuka wake kumekuja baada ya taarifa za awali kudai kuwa bibiye huyo amepoteza maisha baada ya kupata ajali mbaya ya gari.
“Tafadhali, eleweni kwamba niko hai. Sikupata ajali yotote na niko salama kabisa,” amesema na kuongeza kuwa mashabiki wake wanapaswa kuwa makini na vyanzo vya habari visivyo sahihi.
Aidha, Kadiri amewataka mashabiki wake hao kuzoropoti kwenye mamlaka akaunti za mitandao ya kijamii zinazosambaza taarifa za uongo.


