HAGUE, Uswis
ALIYEKUWA Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), Karim Khan, ameondoshwa kwenye nafasi hiyo.
Ni baada ya nchi wanachama kukutana jana Julai 24,2026 na kupiga kura ya kumtoa kwenye kiti hicho baada ya shutuma za udhalilishaji wa kingono dhidi ya mwanamke aliyekuwa msaidizi wake.
Khan, ambaye ni Mwendesha Mashitaka Mkuu wa tatu katika historia ya ICC, alisimishwa kazi mwezi Juni, 2026 ili kupisha uchunguzi juu ya tukio hilo.
Kwa mujibu wa Khan, hakuna kosa alilofanya, huku wanasheria wake wakisema kesi dhidi yake ni zao la siasa za kumchafua.
Wakati huo huo, wengi wanaona kilichomkuta ni matokeo ya jitihada zake za kushughulikia mzozo wa Ukanda wa Gaza unaohusisha Israel na Palestina.


