28 C
New York

Emery atarudi kwa staili gani EPL 2026-27?

Published:

LONDON, Uingereza

WAKATI anakabidhiwa mikoba ya kuinoa Aston Villa mwaka 2022, Unai Emery aliikuta timu hiyo ikiwa nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England (EPL).

Ndani ya miaka yake mitatu na nusu aliyokaa kwenye benchi, Emery ameiwezesha Villa kuwa moja ya timu tishio si tu England, bali hata Ulaya kwa ujumla.

Msimu uliopita, Villa ilimaliza ndani ya ‘Top 4’ ya EPL, mara yao ya pili katika misimu mitatu ya hivi karibuni kumaliza ndani ya ‘Top 5’.

Wakati huo huo, Emery raia wa Hispania, aliipa Villa ubingwa wa Ligi ya Europa, taji lao lao kwanza baada ya ukame wa miaka 30.

Je, kocha huyo wa zamani wa Washika Bunduki wa London, Arsenal, ataendeleza moto wake huo msimu ujao (2026-27)?

Mosi, Villa imewauza nyota wake wawili muhimu, Morgan Rogers aliyetimkia Chelsea kwa Pauni milioni 117 na Youri Tielemans aliyejiunga na Manchester United.

Umuhimu wa Tielemans kikosini ulionekana kuanzia Februari hadi Aprili, 2026, ambapo alikosekana kutokana na majeraha. Villa ilishinda mechi mbili pekee kati ya nane za EPL alizokaa benchi.

Moja ya mechi hizo ni ile ya Villa kutandikwa mabao 4-1 na Chelsea, matokeo yaliyokaribia kuiondosha timu hiyo kwenye Top 4. Bila uwepo wake, wastani wa Villa kushinda mechi za Ligi ulishuka kutoka asilimia 53 hadi 41.

Related articles

Recent articles