21.4 C
New York

Rais Hungary anyoosha mikono, akubali kujiuzulu

Published:

BUDAPEST, Hungary

RAIS wa Hungary, Tamas Sulyok, hatimaye amekubali kujiuzulu baada ya shinikizo kubwa kutoka bungeni.

Hatua yake ya kujiweka kando inakuja baada ya Chama cha Waziri Mkuu, Peter Magyar, kutaka Bunge lipitishe sheria ya kumng’oa Sulyok.

Hata hivyo, wachambuzi wa siasa wanaamini alichokifanya Magyar ni katika kuufurahisha utawala uliopita wa Waziri Mkuu Viktor Orban.

Kwa upande wake, Sulyok amekubaliana na sheria mpya ya kumtoa madarakani, licha ya kudai kuwa kumekuwepo na uvunjifu wa utawala wa sheria.

“Mabadiliko yameua demokrasia ya Katiba ya Hungary. Misingi ya uhuru imekiukwa kwa ajili ya nguvu za kisiasa,” amesema.

Related articles

Recent articles