21.4 C
New York

Maswali yanayomsubiri Waziri Mkuu mpya wa Uingereza 

Published:

LONDON, Uingereza 

ATAANZA majukumu yake kama Waziri Mkuu kesho Julai 20, 2026. Andy Burnham aliyekuwa Meya wa Manchester, Jiji lililoko Kaskazini mwa England. 

Amekuwa Meya wa Manchester kwa miaka tisa na sasa anahamia Downing Street akiwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo kwenye siasa za kimataifa.

Burnham anaondoka Manchester akiwa na heshima kubwa kwa namna alivyoweza kupandisha uchumi kwa kiwango kisichozidi matarajio ya Taifa, pia akipunguza umasikini kwa kiasi kikubwa katika wilaya zake.

Ni kutokana na mchango wake huo, haikushangaza kuona akipachikwa jina la ‘King of North’ (Mfalme wa Kaskazini).

Baada ya kushinda Uchaguzi na kuteuliwa kuwa kiongozi mpya wa Chama cha Labour, anachukua nafasi ya Keir Starmer, Waziri Mkuu aliyejiuzulu akiwa amehudumu kwa miaka miwili tu.

Hata hivyo, katika nafasi yake mpya katika siasa za Uingereza, Burnham anakabiliwa na maswali kadhaa ya kuyapatia majibu katika uongozi wake kama Waziri Mkuu.

Mosi, atafanikiwa kwa namna gani kurejesha uhusiano wa Uingereza na Marekani chini ya Rais Donald Trump?

Katika mahojiano yake baada ya Burnham kutajwa kuwa ndiye Waziri Mkuu mpya wa Uingereza, Trump alitoa kauli tata, akisema hamfahamu kabisa. “Simjui. Ni Meya wa jiji dogo.”

Kauli hiyo inathibitisha kuwa uhusiano mzuri uliokuwepo kati ya nchi hizo umeanza kuyumba.

Kwa miaka mingi, Marekani na Uingereza zimekuwa zikishirikiana si tu kiuchumi, bali pia katika eneo la usalama. 

Hata hivyo, uhusiano huo ulionekana kuyumba wakati wa Waziri Mkuu aliyeondoka madarakani, Starmer, ambaye alikorofishana na utawala wa Rais Trump.

Ni baada ya Starmer kuikatalia Marekani ombi la kutumia kambi zake za kijeshi katika kuishambulia Iran. Rais Trump alikerwa na kitendo hicho.

Pili, Burnham ataendelea kuipinga Israel au atabadili msimamo na kuwaunga mkono washirika hao wa Marekani?

Waziri Mkuu huo anafahamika kwa msimamo wake juu ya mzozo wa Ukanda wa Gaza kati ya Israel na Palestina.

Kwa upande wake, haiungi mkono Israel. Amekiri kuwa Uingereza ilifanya kosa kubwa kuunga mkono operesheni za kijeshi zinazoendelea Gaza.

Tatu, ataendelea kuiunga mkono Ukraine katika vita vyake na Urusi? Ameweka wazi kuwa Ukraine itegemee hilo, kama ilivyokuwa chini ya Waziri Mkuu aliyepita.

Itakumbukwa, Starmer akishirikiana na viongozi wenzake wa Ufaransa na Ujerumani waliunda umoja wao kuiunga mkono Ukraine.

Related articles

Recent articles