KYIV, Ukraine
HATUA ya Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, kumuweka kando aliyekuwa Waziri wa Ulinzi, Mykhailo Fedorov, imezua mjadala ndani ya jeshi la nchi hiyo.
Baadhi ya wanajeshi hawajavutiwa na kukubaliana na uamuzi huo wa kumwacha Fedorov katika Baraza jipya la Mawaziri lililotangazwa na Rais Zelenskyy.
Taaria hiyo ya kushitua inakuja wakati ambao tayari ‘kutumbuliwa’ kwa Fedorov kumezua maandamano makubwa ya raia katika maeneo mbalimbali nchini Ukraine.
Kwa wengi, Fedorov amejijengea taswira ya ushupavu, hasa kwa mikakati yake katika vita vyao dhidi ya Urusi vilivyoanza mwaka 2022.
Hata hivyo, hatua ya mpasuko jeshini inakuja wakati tayari taasisi hiyo imeonywa mara kadhaa kujihusisha na siasa.


