23.6 C
New York

Marekani yaipiga Iran kwa mara ya saba

Published:

TEHRAN, Iran

JESHI la Marekani limetibitisha kufanya shambulizi la usiku kwa mara ya saba mfululizo nchini Iran.

Huo ni mwendelezo wa Iran kushambuliwa usiku tangu Rais Donald Trump alipotangaza kuwa hakuna tena usitishaji wa vita.

Katika taarifa yake baada ya shambulizi la usiku wa kuamkia leo Julai 18, 2026, Marekani imedai kulenga maeneo nyeti ya Taifa hilo, yakiwamo machimbo ya uhifadhi wa silaha.

“Vikosi vya jeshi la Marekani vilitumia ndege za kivita, ndege zisizo na rubani, meli za kivita na baadhi ya silaha zingine,” imeeleza taarifa ya jeshi hilo.

Kwa upande wake, Iran nayo imejibu mapigo kwa kuzishambulia nchi zenye ushirika na Marekani, ikiwamo Kuwait.

Katika hatua nyingine, jeshi la Jordan limekiri kuziona ndege za kivita za Iran kwenye rada zake, ingawa hazikufanikiwa kushambulia.

Related articles

Recent articles