MADRID, Hispania
STRAIKA wa zamani wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang, amejiunga na Deportivo La Coruna ya Ligi Kuu ya Hispania (La Liga).
Nyota huyo raia wa Gabon aliwahi kukipiga La Liga akiwa na Barcelona na sasa amerudi na kusaini miaka miwili na Deportivo.
Aubameyang amejiunga na klabu hiyo baada ya kuachwa na Marseille katika mipango yao ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1).
Deportivo imerejea La Liga baada ya kumaliza msimu wa 2025-26 ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Daraja la Kwanza ya Hispania.
Taarifa zinaeleza kuwa wametumia kitita cha euro milioni 1.5 kuinasa saini ya staa huyo wa zamani wa Borussia Dortmund.


