Na Imani Nathaniel, Gazetini
Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel Tanzania imezindua rasmi ushiriki wake katika maonyesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, Sabasaba kwa kuwasilisha uzoefu wa kipekee wa kidijitali kupitia banda lake.
Uzinduzi huo una kaulimbiu “Teknolojia kutoka ikiendelea kudhihirisha dhamira yake ya kuendeleza mageuzi ya kidijitali nchini Tanzania kwa kutoa huduma bunifu za mawasiliano, intaneti na huduma za kifedha zinazorahisisha maisha ya wananchi na kuchochea ukuaji wa uchumi.
Ukifika katika banda la Halotel, wageni watapata fursa ya kujionea teknolojia na suluhisho mbalimbali za kisasa, ikiwemo huduma ya mtandao wa 5G, HaloFibre, suluhisho za kidijitali kwa biashara na huduma za kifedha za HaloPesa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ushiriki wa Halotel katika maonesho hayo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Halotel Tanzania, Abdallah Salum, amesema kuwa.
“Saba Saba inatupatia jukwaa muhimu la kukutana ana kwa ana na wateja wetu, kusikiliza mahitaji yao na kuonesha ubunifu unaoendelea kuboresha maisha yao kupitia teknolojia.”

Naye Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel Tanzania, Tran Thi Thuy Dung, amesema kampuni itaendelea kuwekeza katika ubunifu ili kuharakisha mageuzi ya kidijitali nchini.
“Halotel inaendelea kujitolea kuwekeza katika suluhisho bunifu zinazoboresha uzoefu wa wateja na kuharakisha mageuzi ya kidijitali nchini Tanzania. Kupitia maonyesho haya, tunawapa wageni nafasi ya kushuhudia kwa vitendo huduma zetu na kuona athari zake halisi katika maisha ya kila siku.”
Kwa upande wake, Meneja wa Masoko wa HaloPesa, Aidat Lwiza, amesema maadhimisho ya miaka 10 ya huduma hiyo yameambatana na ofa na zawadi maalum kwa wateja.

“Kuelekea maadhimisho ya miaka 10 ya HaloPesa, tunafuraha kuwaletea wateja wetu ofa na uzoefu wa kipekee utakaowezesha watu wengi zaidi kufurahia huduma za kifedha kidijitali zilizo salama, rahisi na zenye uhakika katika kipindi chote cha maonyesho ya Saba Saba, ” amesema
Aidha kuelekea maadhimisho ya miaka 10 ya HaloPesa, Halotel imeandaa ofa maalum, zawadi mbalimbali na shughuli za kuwashirikisha wateja, zikiwa na lengo la kuboresha zaidi uzoefu wa wageni watakaotembelea banda hilo katika kipindi chote cha maonyesho.


