30.1 C
New York

Canada yatua 16 Bora ikiitoa Afrika Kusini

Published:

TORONTO, Canada

TIMU ya soka ya Taifa ya Canada imekuwa ya kwanza kuingia hatua ya 16 Bora baada ya kuitoa Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’.

Katika mchezo huo wa 32 Bora uliochezwa mjini Houston, Marekani jana Juni 29, 2026, Canada ilishinda bao 1-0, mfungaji akiwa ni Stephen Eustaquio.

Afrika Kusini inaondoka ikiwa tayari ina rekodi ya kuvuka hatua ya makundi kwa mara ya kwanza katika historia ya Kombe la Dunia.

Kwa matokeo hayo, Canada ya kocha Jesse Marsch itakutana na mshindi kati ya Morocco na Uholanzi siku sita zijazo.

Je, Canada itatoboa katika hatua inayofuata endapo itakutana na moja ya timu hizo?

Related articles

Recent articles