12.9 C
New York

Kiti cha Katibu Mkuu UN: Nani alifaulu, nani alifeli?

Published:

NEW YORK, Marekani

KATIBU Mkuu ndiyo cheo cha ngazi ya juu zaidi ndani ya Umoja wa Mataifa (UN) na kwa sasa kinashikiliwa na Waziri Mkuu wa zamani wa Ureno, Antonio Guterres.

Guterres, ambaye atamaliza muda wake Desemba, 2026, na Katibu Mkuu mpya kuanza kazi Januari Mosi, 2027, ni mtu wa 10 kushika nafasi hiyo.

GLADWYN JEBB (1945-1946)

Mwanadiplomasia huyo wa Uingereza ndiye Katibu Mkuu wa kwanza wa UN, akishika kwa miezi takribani mitatu nafasi hiyo kuanzia Oktoba 24, 1945, hadi Februari Mosi, 1946.

Kwa kuwa Jebb alikalia kiti hicho baada ya kumalizika kwa Vita vya Pili vya Dunia, moja ya majukumu yake ilikuwa ni kuimarisha hali ya usalama kwa kusimamia usawa na uhuru kwa nchi zilizokuwa chini ya ukokoni.

TRYGVE LIE (1946-1954)

Raia huyo wa Norway alitangazwa kuwa Katibu Mkuu wa Norway kuazia Februari Mosi, 1946, hadi Novemba 10, 1952. Akiwa kwenye nafasi hiyo, Li alisifika kwa uwezo wake wa kutatua migogoro mingi ya kimataifa.

Chini ya uongozi wake, UN ilimaliza Vita vya Korea (1950 – 1953), Vita vya India na Pakistan (1949), Vita ya kupigania uhuru nchini Indonesia (1945-1950), na Vita vya China (1949).

DAG HAMMARSKJOLD (1953 – 1961)

Huyo ni mwanadiplomasia wa Sweden aliyeshika nafasi ya Katibu Mkuu wa UN kuanzia Aprili 10, 1953, hadi Septemba 18, 1961). Anatajwa kuwa mmoja ya waliofanikiwa zaidi katika kiti hicho.

Hammarskjold aliimarisha kwa kiasi kikubwa uhusiano wa Israel na mataifa ya Kiarabu. Alisimamia makubaliano ya Marekani na China kuachia wafungwa waliotokana na Vita vya Korea. Akitoka kusukuhisha mgogoro wa Congo, ndege yake ilipata ajali, akafariki na abiria wengine 14.

U THANT (1961-1971)

Baada ya kukaimu kwa muda kiti cha Hammarskjold, Thant raia wa Burma, alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu kuanzia Novemba 30, 1961, hadi Desemba 31, 1971).

Moja ya mafanikio yake ni kuzima vita ya nyuklia iliyokaribia kuanza kati ya Marekani na Umoja wa Kisoviet mwaka 1962. Pia, alizima vita iliyokaribia kulipuka kati ya Uturuki na Ugiriki.

KURT WALDHEIM (1972 – 1981)

Akiwa Katibu Mkuu kuanzia Januari Mosi, 1972, hadi Desemba 31, 1981, raia huyo wa Austria aliratibu operesheni nyingi za kulinda amani Sudan, Namibia, Yemen, Angola, Guinea, na Mashariki ya Kati.

Ni wakati huo, Waldheim alifanya ziara nyingi na za kimkakati katika nchi za Syria, Lebanon, Israel, Misri na Jordan kwa lengo la kuimarisha hali ya usalama.

JAVIER PEREZ DE CUELLAR (1982 – 1991)

Ni mwanadiplomasia wa Peru na historia itamkumbuka kwa kumaliza Vita Baridi baada ya kuingia madarakani kuanzia Januari Mosi, 1982, hadi Desemba 13, 1991.

Mbali na mafanikio mengine, alimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Cambodia, alisimamia mchakato wa Namibia kupata uhuru, pia akimalia Vita kati ya Iran na Iraq (1980 – 1988).

BOUTROS BOUTROS-GHALI (1992 – 1996)

Januari Mosi, 1992, UN ilimtangaza mwanadiplomasia huyo wa Misri kuwa Katibu Mkuu. Aliiongoza hadi Desemba 31, 1996. Kuchaguliwa kwake kulitokana na shinikizo la nchi za Afrika kutaka nazo ziwe na historia ya kuwa na Katibu Mkuu wa Umoja huo.

Chini ya uongozi wake, ndipo Afrika iliposhuhudia mauaji ya kimbari nchini Rwanda. Boutros-Ghali anakosolewa kwa uongozi wake kushindwa kuchukua hatua wakati huo.

KOFI ANNAN (1997 – 2006)

Huyo ni mwanadiplomasia mkongwe raia wa Ghana. Akiingia madarakani Januari Mosi, 1997, na kumaliza Desemba 31, 2006. Anatajwa kuwa na mafanikio makubwa kwenye nafasi hiyo.

Alisifika kwa mikakati ya kudhibiti Ukimwi, kupigania haki za binadamu, kulaani vitendo vya rushwa, hasa barani Afrika. Pia, kwa mchango wake katika kuimarisha hali ya usalama, alipewa tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 2001.

BAN KI-MOON (2007 – 2016)

Mwanadiplomasia raia wa Korea Kusini, ambaye aliiongoza UN katika nafasi ya Katibu Mkuu kuanzia Januari Mosi, 2007, hadi Desemba 31, 2016.

Ban Ki-Moon alifisika kwa mikakati yake ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani, ingawa utawala wake ulishuhudia Marekani ikiivamia Iraq (2003 – 2021), vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria (2011), na kuuawa kwa Muammar Gaddafi (2011).

GUTERRES (2017 – 2026)

Aliingia madarakani Januari Mosi, 2017, na utawala wake umegubikwa pia na migogoro mingi; Urusi na Ukarine, Israel na Palestina, Armenia na Azerbaijan, na Marekani/Israel na Iran.

Oktoba 2, 2024, Serikali ya Israel ilimshutumu kwa madai kuwa hakulaani shambulizi la Iran dhidi yao. Chini yake, UN iliidhinisha Dola bilioni 22.7 kwa ajili ya misaada ya kibinadamu katika maeneo yenye migogoro duniani.

Related articles

Recent articles