21.9 C
New York

Uchambuzi Kundi la Stars kufuzu AFCON 2027

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

WENYEJI wa fainali za Mataifa ya Afrika za mwakani (AFCON 2027), Taifa Stars, wameangukia Kundi L wakati wa droo ya upangaji wa makundi ya mechi za kufuzu iliyochezeshwa hivi karibuni mjini Cairo, Misri.

Mechi za kuwania tiketi zitaanza kuchezwa kati ya Septemba, 2026, na Marchi, 2027, huku fainali zenyewe zikitarajiwa kuanza Juni 19 na kumalizika Julai 17.

Katika Kundi lake, Stars imepangwa na mataifa ya Nigeria, Madagascar na Guinea-Bissau, huku zikiwa ni timu mbili pekee zinazotakiwa kuvuka na kuingia 16 Bora.

Stars ya Tanzania ni mwenyeji wa mashindano hayo kwa kushirikiana na majirani zake, ‘Harambee Stars’ (Kenya) na ‘The Cranes’ (Uganda).

Katika Kundi hilo, ‘Super Eagles’ (Nigeria) inapewa nafasi kubwa ya kumaliza kileleni, hiyo ikitokana na ubora wa wachezaji, kiwango cha timu na nafasi yake katika viwango vya FIFA (Shirikisho la Soka la Kimataifa).

Eagles wanashika nafasi ya 26 duniani, wakati Madagascar ni ya 104, Stars ni ya 113 na Guinea ni ya 132 katika viwango hivyo vya ubora wa kandanda.

​Stars itacheza mechi za kuwania tiketi kama sehemu ya maandalizi tu kwani tayari imeshajihakikishia nafasi ya kushiriki kwa tiketi ya uenyeji, kama ilivyo kwa Kenya (Kundi H) na Uganda (Kundi D).

Hivyo, kwa kuwa Stars ina uhakika, Kundi L linatafuta timu nyingine moja ya kwenda nayo kwenye mashindano hayo makubwa zaidi kwa ngazi ya timu za taifa barani Afrika.

​Kwamba hata kama itatokea kwa Stars kuburuza mkia, bado itakuwa imefuzu, ikiiungana na timu iliyomaliza mechi zake ikiwa kileleni mwa msimamo wa Kundi L.

​Wakati Eagles ikionekana kuwa na nafasi kubwa, ‘Barea’ (Madagascar) ni tishio kubwa kwao. Ikumbukwe, Kisiwa hicho kimefuzu fainali zijazo za Juni 11, 2026.

Related articles

Recent articles