9.5 C
New York

Klabu 16 kuchuana mashindano ya Taifa ya kuogelea kesho

Published:

Na Mwandishi Wetu

JUMLA ya klabu 16 za mchezo wa kuogelea kutoka ndani na nje ya Tanzania zinatarajia kushiriki mashindano Taifa yatayoanza kesho Aprili 10-12, 2026 katika bwawa la kuogelea la Shule ya Kimataifa ya Tanganyika(IST), Masaki, jijini Dar es Salaam.

Kati ya klabu hizo 14 zinatoka Tanzania, moja kutoka Zambia na nyingine inatoka Kenya, ambapo jumla ya waogeleaji wanatarajiwa kuwa 190.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Elimu na Maendeleo wa Chama Cha Kuogelea  Tanzania (TSA),  Jeremiah Keema, mashindano hayo ni muhimu kwani yatatumika kama mashindano ya kufuzu kwa ajili ya Mashindano ya Dunia ya Kuogelea yatakayofanyika nchini China Desemba 2026.

Amesema katika mashindano ya dunia Tanzania itawakilishwa na waogeleaji wanne, wanaume wawili na wanawake wawili.

“Pia mashindano ya Taifa yanalenga kukuza kiwango cha mchezo wa kuogelea nchini, kutoa fursa kwa waogeleaji kuonyesha vipaji vyao, pamoja na kupata wawakilishi watakaoipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika mashindano ya kimataifa,”

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img