13.5 C
New York

Anguko la Leicester City kutoka ubingwa EPL hadi ‘mchangani’

Published:

LONDON, Uingereza

MIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliushangaza ulimwengu wa soka walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL). Walifanya hivyo msimu wa 2015-16.

Kwa sasa, timu hiyo iko kwenye hali mbaya huko Championship (Ligi Daraja la Kwanza England), ambapo wanapigania kujinasua katika janga la kuangukia League One (Daraja la Pili).

Ikiwa nafasi ya 20 katika msimamo wa Championship, Leicester City imeshinda mechi 10 pekee kati ya 30 ilizoshuka dimbani msimu huu.

Ni kutokana na mwenendo huo mbaya, mabosi wa klabu hiyo walikubaliana kumfuta kazi kocha raia wa Hispania, Marti Cifuentes. Alitimuliwa Januari, 2026.

Cifuentes alikuwa kwenye uhusiano mbaya na mashabiki, ambao mfululizo wa matokeo mabaya ulisababisha wagome kushangilia ushindi wao wa mabao 2-1 dhidi ya West Brom.

Hivi karibuni, Leicester City ilishukiwa na rungu la kukatwa pointi sita kwa kosa la kukiuka Sheria ya Nidhamu ya Matumizi ya Fedha (Financial Fair Play).

Awali, adhabu hiyo ilipaswa kuwa ni pointi 12, sambamba na faini ya kitita cha Pauni milioni 20, ambazo zingeifilisi kabisa klabu hiyo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img