Na mwandishi wetu, Gazetini
NDIYE aliyefunga mabao yote katika ushindi wa 2-0 walioupata Yanga ‘Timu ya Wananchi’ katika mchezo uliopita dhidi ya Cosmo Politan.
Ulikuwa ni mchezo wa hatua ya 64 Bora ya Kombe la Shirikisho, ambapo Buba Jammeh aliondoka uwanjani akiwa amebakiza bao moja kuondoka na ‘hat trick’.
Je, Buba ni nani? Makala haya yanakufunulia usiyoyajua kuhusu mshambuliaji huyo aliyesajiliwa kupitia dirisha dogo la usajili.

Mosi, nyota huyo anayetajwa kuwa na umri wa miaka 24, japo vyanzo vingine vinataja 33, ametua Jangwani akitokea Interclube ya Ligi Kuu nchini Angola.

Pili, Buba ni raia wa Gambia, ingawa pia anao wa Angola alikoishi na kucheza soka kwa miaka mitano.
Tatu, hadi anatua Yanga alishacheza mechi saba za Ligi Kuu ya Angola, ambapo alifunga bao moja.
Nne, ni kiungo wa pembeni, ambaye ukiacha kasi na uwezo wa chenga, pia anatumia miguu yote miwili, hivyo anaweza kutokea kushoto au kulia. Hiyo itategemea na mipango ya benchi la ufundi.
Je, Buba atauendeleza moto aliounesha katika mchezo dhidi ya Cosmo Politan? Ni mwanzo wa safari ya mafanikio yake Ligi Kuu Bara?


