13.9 C
New York

Lai wa Hong Kong ahukumiwa miaka 20 gerezani

Published:

HONG KONG, China

MFANYABIASHARA tajiri mjini Hong Kong, Jimmy Lai, amehukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani baada ya Mahakama kumkuta na hatia.

Awali, lilikuwepo tishio la Lai mwenye umri wa miaka 72 kuhukumiwa kifungo cha maisha, akitajwa na Mahakama kuwa chanzo cha tishio la usalama wa Taifa kwa kuchochea chuki dhidi ya Serikali ya China.

Bilionea huyo ambaye pia ana uraia wa Uingereza, amekuwa mkosoaji wa mamlaka za Beijing, akizishutumu mara kadhaa kwa kuingilia uhuru wa Hong Kong.

Mbali ya Lai, pia wafanyakazi wake sita wa zamani wa Gazeti lake la Apple Daily nao wamehukumiwa vifungo vya kati ya miezi tisa na miaka 10 gerezani.

Mamlaka za Beijing zinamtaja Lai kuwa ni msaliti, licha ya tajiri huyo kusisitiza kuwa hajafanya kosa zaidi ya kutetea masilahi ya watu wa Hong Kong.

Wakati huo huo, wanasheria wake wameendelea kusisitiza kuwa Lai anapitia kipindi kigumu akiwa gerezani kwani afya yake imedorora.

Katika taarifa yao ya utetezi dhidi ya hukumu iliyotolewa na Mahakama, wamesema anasumbuliwa na maradhi ya shinikizo la damu na kisukari.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img