8 C
New York

Serikali yaendelea na maandalizi ujenzi reli ya Kusini

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

SERIKALI kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC) imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa awali kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kiwango cha kisasa (SGR) kutoka Mtwara hadi Mbambabay pamoja na matawi yake ya Liganga na Mchuchuma, yenye jumla ya urefu wa takribani kilomita 1,000.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye, bungeni jijini Dodoma.

Mbunge huyo alitaka kujua iwapo Serikali ina mpango wa kuanza upembuzi wa ujenzi wa reli ya SGR kutoka Dar es Salaam hadi mikoa ya Kusini, ikizingatiwa kuna maandalizi ya utekelezaji wa Mradi wa Gesi Asilia (LNG).

Akijibu swali hilo, Kihenzile amesema kwa sasa Serikali inaendelea na juhudi za kutafuta rasilimali fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa, ikiwemo kutumia utaratibu wa ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP).

Aidha, amesema reli ya kutoka Dar es Salaam hadi Mtwara imetambuliwa kuwa na umuhimu mkubwa katika mpango kabambe wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuwa itaunganisha Bandari ya Dar es Salaam na Bandari ya Mtwara na kuchangia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi, maendeleo ya kijamii na kuimarisha mtangamano wa kikanda.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img