TOKYO, Japan
TETSUYA Yamagami ambaye ni mshitakiwa wa mauaji ya Waziri Mkuu wa zamani wa Japan, Shinzo Abe, amehukumiwa kifungo cha maisha.
Yamagami amekuwa chini ya ulinzi tangu mwaka 2022, muda mfupi tu baada ya kumuua kwa kumpiga risasi ya kichwa Abe.
Kwamba ni takribani miaka mitatu na nusu imepita tangu alipofanya mauaji hayo karibu na Mji wa Nara.
Watu zaidi ya 700 walikusanyika nje ya Mahakama ya Wilaya ya Nara leo Januari 20, 2021 kufuatilia hukumu yake.
Wakati huo huo, hukumu yake imezua hisia mseto, ambapo wapo wanaoamini kuwa malezi aliyokulia ndiyo yaliyosababisha atekeleze mauaji hayo.


